Klabu ya PSG ya Ufaransa na Arsenal kutoka Uingereza wataingia uwanjani kutafuta tiketi ya kufuzu katika fainali ya michuano ya klabu bingwa Ulaya. Hii ni mechi ya nusu fainali ya mkondo wa pili. PSG wanaongoza mtanange huu baada ya ushindi wa bao moja kwa nunge katika mechi ya kwanza.